Description
Suki ni mwanafunzi wa darasa la sita ambaye alikuwa akihifadhi akiba yake ili kununua kitabu cha picha za wanyamapori wakati wa likizo. Hata hivyo, kabla ya siku ya ununuzi kufika, tukio la kushtua linatokea. Mwizi anaingia nyumbani kwao Suki na kuiba kisanduku chake cha kuhifadhi pesa na vitu vingine vya thamani. Polisi wanaarifiwa kuhusu tukio hilo, lakini juhudi zao za kumkamata mwizi hazifaulu. Suki anachukua jukumu la kufanya upelelezi mwenyewe ili kugundua ni nani aliyeiba kisanduku chake. Je, atafanikiwa katika juhudi zake?
Reviews
There are no reviews yet.